HABARI MPYA

Friday, May 28, 2021

MKUTANO WA 49 WA KAMATI YA KITAIFA YA UWEZESHAJI NA URAHISISHAJI WA USAFIRI WA ANGA NCHINI WAFANYIKA ZANZIBAR

 

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali (katikati),Mkurugenzi Mkuu wa TCAA na wanakamati ya kitaifa ya uwezeshaji na urahisishaji wa usafiri wa anga nchini kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa 49 wa kamati hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa 49 kamati ya kitaifa ya uwezeshaji na urahisishaji wa usafiri wa anga nchini 


Kamati ya kitaifa ya uwezeshaji na urahisishaji wa usafiri wa anga nchi imekutana katika mkutano wa 49 wa kamati hiyo uliofanyika mjini Unguja visiwani Zanzibar na kupata baraka za ufunguzi kutoka kwa waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Rahma Kassim Ali.

Akizungumza wakati wa hotuba yake,Mhe.Rahma Kassim Ali aliwahimiza wajumbe wa kamati hiyo kufanya kazi kwa bidii na kutanguliza uzalendo katika kutafuta suluhu na kujadili namna ya kutatua changamoto zinazokabili sekta ya usafiri wa anga kwani ni chanzo muhimu cha mapato ya nchi.

“Nashukuru kwa mualiko wa ufunguzi wa mkutano huu muhimu sana unaokutanisha wadau wa usafiri wa anga nchini.Nina imani kubwa kuwa utakwenda kuwa na tija zaidi katika kupunguza na kutatua changamoto mbalimbali na bila shaka kuimarisha uchumi wa taifa letu”, ameeleza  Mhe.Rahma Kassim Ali

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bw.Hamza S. Johari akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 49 kamati ya kitaifa ya uwezeshaji na urahisishaji wa usafiri wa anga nchini 

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA) Bw.Hamza S. Johari amesema kamati hii imejikita zaidi katika utekelezaji wa sheria na mkataba wa usafiri wa anga wa kimataifa maarufu kama mkataba wa Chicago wa mwaka 1944 unaotaka katika masuala ya abiria na mizigo wanapopita katika uwanja wa ndege kuwe na urahisi, usalama, ufanisi na kwa haraka bila ya kuwa na ucheleweshaji sana kwa abiria na mizigo pasipo kuwa na sababu za msingi.

“Lengo kubwa la mkutano huu ni kuziangalia changamoto zinazoleta uchelewashaji kwa abiria na mizigo katika viwanja vyetu vya ndege na kuja na hatua zitakazo leta urahisi na faraja kwa abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini”, amefafanua Bw. Johari

Sambamba na hilo Bw. Johari amesisitiza kuwa usafiri wa anga hauruhusu upitishaji wa vitu haramu kama vile madawa ya kulevya na kwamaana hiyo inawahusisha na kushirikiana na wadau wote wanaohusika ili kuhakikisha hilo linafanyika ili kuendelea kuilinda taswira ya nchi yetu.

Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo,  Bw.Daniel N. Malanga amesema kuwa mkutano huu unatoa fursa ya kipekee kwa wadau wa sekta ya usafiri wa anga nchini kukutana pamoja kujitathini, kujadiliana na kuja na mapendekezo yatakayoenda kuleta maboresho, unafuu na kuimarisha sekta ya anga hapa nchini.

 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji na Urahisishaji wa Usafiri wa Anga nchini,Bw.Daniel N. Malanga akitoa neno la ukaribisho kwa waliohudhuria mkutano wa 49 kamati ya kitaifa ya uwezeshaji na urahisishaji wa usafiri wa anga nchini 

“Kamati hii ni mtambuka hivyo inatoa fursa ya kujadili changamoto mbalimbali kwa upana kwani inajumuisha wadau mbalimbali wa usafiri wa anga nchini. Kwahiyo katika mkutano huu tutajadili kwa kina changamoto zinazokikabili kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA)”, amesisitiza Bw. Malanga

Katika hatua nyingine, kamati imefanya ziara katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar (AAKIA) na kujionea namna shughuli zinavyofanyika kwenye jengo la pili la abiria (Terminal 2).

Aidha, pamoja na hayo kamati imetembelea jengo jipya la abiria (Terminal 3) ambalo linatarajia kuanza kuhudumia wasafiri ifikapo Julai Mosi mwaka huu.

Vilevile, pamoja na changamoto walizozibaini kamati imeipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua iliyofikia katika ujenzi wa jengo hilo la abiria linalotarajia kuhudumia makadirio ya abiria milioni moja na nusu kwa mwaka.

Mkutano huu unafanyika mara mbili kwa mwaka na unahusisha wadau wa usafiri wa anga wakiwemo Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA),Mamlaka za Viwanja vya Ndege (TAA na ZAA),Idara za Kiusalama katika viwanja vya ndege,wadau wa mazingira na watoa huduma kwenye viwanja vya ndege nchini.

Kwa mwaka huu, mkutano umefanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 27 hadi 28 Mei, 2021.


Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Uwezeshaji na Urahisishaji wa Usafiri wa Anga nchini wakiwa kwenye ziara katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume  kujionea namna shughuli zinavyofanyika uwanjani hapo














Sunday, January 26, 2020

TCAA YAENDELEA KUWAJENGEA UWEZO KUPENDA SEKTA YA ANGA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI MIKOA YA KIGOMA NA KAGERA

Mkufunzi Mkuu Kitengo cha huduma za viwanja vya ndege kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) kilichopo Dar es Salaam Bi. Thamarat Abeid akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Katubuka na Kirugu zilizopo mkoani Kigoma.   
Mkufunzi Mkuu Kitengo cha huduma za viwanja vya ndege kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) kilichopo Dar es Salaam Bi.Thamarat Abeid akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Rugambwa na Ihungo zilizopo mkoani Kagera.

Wednesday, January 22, 2020

WARSHA MASHULENI, MKOA WA TABORA

Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kituo cha Tabora Bw.Daniel Nyimbo  akielezea jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo.

Sehemu ya wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo wakisikiliza maelekezo kutoka kwa wataalamu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.


Mkufunzi Mkuu kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) kilichopo Dar es salaam Bi.Thamarat Abeid  akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo.

Picha ya pamoja baada ya warsha

Wanafunzi wa shule ya sekondari Milambo wakijiandaa kushiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo.


Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kituo cha Tabora Bw.Daniel Nyimbo  akielezea jambo kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Milambo walioshiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo.

Mkufunzi Mkuu kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) kilichopo Dar es salaam Bi.Thamarat Abeid  akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Milambo walioshiriki warsha hiyo.

Picha ya pamoja baada ya warsha



Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), leo, 22/01/2020. Imeendesha warsha za kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo. Zaidi ya  wanafunzi 600 kutoka shule ya sekondari Mirambo, Tabora Boys na Tabora Girls wameshiriki  Warsha hiyo.

Wednesday, December 11, 2019

KIKAO CHA KUPITIA MAOMBI YA LESENI ZA UENDESHAJI BIASHARA YA USAFIRI WA ANGA




Wadau wa Sekta ya Usafiri wa Anga nchini, wakishiriki kikao cha kupitia maombi ya leseni za uendeshaji biashara ya Usafiri wa Anga, Makao Makuu ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Banana Ukonga. Kampuni zimeshiriki kuleta maombi ya kupewa leseni za kuendesha biashara ya Usafiri wa Anga. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi TCAA, Prof.Longinus Rutasitara.

Saturday, December 7, 2019

TCAA YAWATUNUKU WASHINDI WA SHINDANO LA KUANDIKA INSHA KUHUSU MASUALA YA USAFIRI WA ANGA

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Vallery Chamulungu akitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza Albert Dida kutoka shule ya msingi Libermann katika shindano la insha lililoandaliwa na TCAA kwa lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi na kuamsha hali ya kujifunza juu ya masuala mbali mbali ya usafiri wa anga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usafiri wa anga duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason/MMG.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Vallery Chamulungu akitoa zawadi kwa mshindi wa kwanza Yvonne Lyaruu katika shindano la insha lililoandaliwa na TCAA kwa lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi na kuamsha hali ya kujifunza juu ya masuala mbali mbali ya usafiri wa anga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usafiri wa anga duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Chuo cha Usafirishaji ambaye alikuwa Jaji Mkuu wa shindano la insha (Mchango wa Shirika la Ndege la Taifa Katika Uchumi wa Nchi) Bw. Abubakari Nuru akitoa neno wakati akisoma washindi wa shindano la insha lililoandaliwa na TCAA kwa lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi na kuamsha hali ya kujifunza juu ya masuala mbali mbali ya usafiri wa anga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usafiri wa anga duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa Chuo cha Usafirishaji ambaye alikuwa Jaji Mkuu wa shindano la insha (Mchango wa Shirika la Ndege la Taifa Katika Uchumi wa Nchi) Bw. Abubakari Nuru akitoa neno wakati akisoma washindi wa shindano la insha lililoandaliwa na TCAA kwa lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi na kuamsha hali ya kujifunza juu ya masuala mbali mbali ya usafiri wa anga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usafiri wa anga duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Vallery Chamulungu.
Mshindi wa kwanza Albert Dida akiwasilisha mada yake.
Mshindi wa Pili Yvonne Lyaruu akiwasilisha mada yake.
Mshindi wa tatu Alpha Tito akiwasilisha mada yake.
Meza ya majaji wakifuatilia shindano hilo.
Wafanyakazi wa TCAA na wanafunzi wa shule mbali mbali za Dar es Salaam wakifuatilia shindano.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Vallery Chamulungu (wa pili toka kushoto).
Mzazi akitoa shukrani mara baada ya kumalizika kwa shindano.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Vallery Chamulungu akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano la insha lililoandaliwa na TCAA kwa lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi na kuamsha hali ya kujifunza juu ya masuala mbali mbali ya usafiri wa anga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usafiri wa anga duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Washindi wa shindano la insha lililoandaliwa na TCAA kutoka kulia ni Hazafa Amirali, Moureen Silayo, Alpha Tito, Yvonne Lyaruu na Albert Dida.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Vallery Chamulungu (wa tatu toka kulia mstari wa nyuma) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji na washindi wa shindano la insha lililoandaliwa na TCAA kwa lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi na kuamsha hali ya kujifunza juu ya masuala mbali mbali ya usafiri wa anga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usafiri wa anga duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam. (Mstali wa mbele) washindi hao ni (kutoka kulia) Hazafa Amirali, Moureen Silayo, Alpha Tito, Yvonne Lyaruu na Albert Dida.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Vallery Chamulungu (wa tatu toka kulia mstari wa nyuma) akiwa katika picha ya pamoja na Majaji, Wazazi  na washindi wa shindano la insha lililoandaliwa na TCAA kwa lengo la kukuza uelewa wa wanafunzi na kuamsha hali ya kujifunza juu ya masuala mbali mbali ya usafiri wa anga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya usafiri wa anga duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Bendera ikipandishwa ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya siku ya usafiri wa anga duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Maandamano ya maadhimisho ya siku ya Anga Duniani.

Tuesday, December 3, 2019

DIRECTOR GENERAL

Please Share This Site